March 7, 2019


IKIWA ni siku tisa tangu kituo cha Utangazaji cha Clouds Media kupata pigo kwa kuondokewa na aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa kituo hicho, Ruge Mutahaba, chombo hicho cha habari kimepata pigo jingine tena leo kwa kuondokewa na mtangazaji wake, Ephraim Kibonde,kilichotokea alfajiri ya leo, Alhamisi, Machi 7, 2019 jijini Mwanza kwa tatizo la presha.

Viongozi wa siasa na mastaa mbalimbali wameeleza hisia zao kufuatia msiba huo.
Hussein Bashe; Innalilahi wainnailayhii Rajiuun. Huu ni msiba mziki kwa Familia ya wanahabari, Poleni Clouds ni Njia yetu sote lakini baada ya Msiba wa Ruge kwenu huu ni Mtihani Allah huwaletea Wajawake Mitihani kuwapima IMANI hii ni njia moja wapo ya kukumbusha na Kupima IMANI watu

Binafsi niwatie moyo clouds lakini pia niwape pole sana Familia na watoto ambao leo tena wamepoteza BABA. Allah amjaalie Pumziko la Amani na kheri huko mbele.

Zitto Kabwe; Nimepokea habari za kifo cha Ephraim Kibonde kwa Masikitiko makubwa sana. Pole zangu kwa familia ya Kibonde na familia ya  kwa msiba huu. Kazi ya Mola haina makosa. Wafiwa wote mungu awapitishe salama Katika mtihani huu mkubwa.
Mwigulu Nchemba; Umetangulia Kaka,Pole Clouds Media,Poleni wanafamilia kwa msiba huu mzito.
Sisi tulikupenda sana, ila Mungu amekupenda zaidi , Pumzika kwa amani kaka yetu na rafiki yetu Ephraime Kibonde , Mungu wa faraja anyooshe mkono wake awape faraja ya kweli familia ya kibonde na Ndugu zetu @cloudsfmtz@cloudstv.
Gerson Msigwa; Inna lillahi wa inna ilayhi raji’un.
Rayvanny; R.I.P BIG BROTHER
AY; Nimestushwa sana na taarifa ya kifo chako Kaka yangu…Pumzika kwa Amani Kaka Yangu #EphraimKibonde…Tumeshirikiana kwenye Mengi ya Kikazi na Familia..Pumzika kwa Amani Wakukaja πŸ™πŸΏπŸ™πŸΏπŸ™πŸΏπŸ™πŸΏ Tusali sana ha-tujui Siku wala Saa
/…Mbele ni giza ila Sala ndio Taa

Jaydee; Hili ni jambo zito kwa watu wenye ukaribu na Ephraim Kibonde. Tunakaa tunakunywa, tunacheka siku nyingine mmoja wetu anatwaliwa πŸ˜­πŸ˜­. Mwenyezi Mungu wa rehema ukawafariji watoto, ndugu, jamaa na marafiki kwa pigo hili. Tunashukuru kwa kila jambo πŸ™πŸ½. RIP my brother (Shemejiiii).

Fid Q; Inna lillah wainna ilaih raajiuun.. #RipKibz
Prof Jay; Daah hii habari Imenishtua sana, R.i.p Kaka EPHRAIM KIBONDE.
Wastara; Mtihani sana wallah, Poleni sana cloudz maana, Mko katika wakati mgumu saana kwakweli unaweza kusema mungu anawaonea kumbe ndivyo alivyoataka iwe poleni sana, Lala salama kibonde.
Nay wa Mitego; Rest In Peace Uncle😭#EfrahimKinonde.

Johari; R.i.p bro tulikupenda mungu amekupenda zaidi. πŸ˜­πŸ˜­πŸ˜­πŸ˜­
Mbasha; Hii ni habari mbaya sana daaaah nimelia aisee miezi kadhaaa tumemzika shemeji juzi tu ulikuwa Mc kwenye msiba wa ruge leo umetutoka nakosa la kuongea kabisa my friend kibonde BWANA ALITOA BWANA AMETWA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE @cloudsfmtz @josephkusaga.

Maulid Kitnge; Tumetoka mbali sana Efrahim Kibonde. Mungu amekuchukua ni kazi yake Mola haina makosa.

Wolper; Kaka yangu usifanye hivyo bhana πŸ˜³πŸ˜³πŸ˜³πŸ’”πŸ’”πŸ’” #Mungu mkali Jamani, #poleni famlia ya clouds Wote jamani hili Ni pigo πŸ™
Kama ujaanza kubadilika Nakumrudia Mungu ,Basi Naomba vdio hii ya kaka yetu marehem,uisikilize nakuiangalia Mara 10,alafu jua kwamba ata yeye Alimsindikiza Boss wake juzi, na kahojiwa juzi,Na naimani akupata ata dakika yakuwaaga watoto wake,Basi Wote Tuseme Amen πŸ™ #R.I.p Broo.

MadeeBrother KIBSπŸ˜­πŸ˜­πŸ™!!! Bt kazi yake mola haina makosa!!
Gabo Zigamba; Swali ni kwamba Roho mbaya wewe itakusaidia nini na itakufikisha wap? Ahsante Mungu kwa kuweka Siri kubwa hata asijue mtu nani anafuata baada ya Marehem.Ikumbukwe kuwa tunaipenda sana Dunia na inatupenda pia lakini Dunia haipendi aliekwenda arudi.   #Mbeleyako#Nyumayetu

Ridhiwani Kikwete; Umauti ni Njia tumetengenezewa ili kuujua Utukufu wa Mwenye Ujuzi, anayeumba, kuamsha na kuhukumu. Kapumzike Ndg yetu. Mwendo Umeupiga…   #RipKibonde#PoleniWanafamiliaCloudsFm#PigoJengine

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic