MWANAMUZIKI wa Kizazi Kipya, Msami Giovan ‘Msami’ amekiri kuwa aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Marehemu Ruge Mutahaba alimtoa kwenye tabia ya wizi na kupora watu.
Akizungumza na Over Ze Weekend, Msami alisema hawezi kueleza ni jinsi gani ameumia na mtu akamuelewa kwani Ruge ndio mtu pekee aliyemfanya mpaka leo asiuawe.
Akiendelea kuzungumza, Msami alisema kipindi hicho alikuwa akiishi maisha ya kihuni Temeke ambapo alikuwa mwizi wa kutupwa na tena wa kuvunja nyumba za watu, kuiba mali na kwenda kuuza lakini anamshukuru sana Ruge ndiyo ameweza kuona kipaji chake na kumwambia aachane na hivyo vitu aimbe.
“Nitalia siku zote juu ya Ruge, ameniepusha na kifo mimi maana jamaa niliyekuwa naiba naye majumbani kwa watu ameshauawa. Baada ya Ruge kuniona na kunichukua nilisafiri kwenda Afrika Kusini na niliporudi nilikuta yule rafiki yangu kauawa kwa sababu ya wizi,” alisema Msami huku akilia kwa uchungu.
Msami aliongeza kuwa, moja ya mafanikio makubwa aliyokuwa nayo ni Ruge kumuamini kuwa msanii na kiongozi wa madansa na pia kumfanikishia kununua gari aina ya Toyota IST (nyeusi) ambayo imekuwa ikimsaidia katika kazi zake za kimuziki.
Huyu amekiri mwenyewe kuhusika na wizi lakini mpaka tutasahau hatafikishwa mahakamani.
ReplyDeleteNaamini hakuna jalada lolote kumhusu huyu
ReplyDelete