BAADA YA KUINGIA MAKUNDI, WACHEZAJI YANGA KUPATA KIFUTA JASHO
Uongozi wa Yanga kupitia Katibu Mkuu wa klabu, Charles Boniface Mkwasa, umetangaza kuwa utawapa kifuta jasho wachezaji wake baada ya kuiwezesha timu kuingia hatua ya makundi.
Yanga wamefikia hatua hiyo ili kuzidi kutoa hamasa kwa wacheza ambao wamesaidia kikosi hicho kuiondosha Wolaita Dicha SC kutoka Ethiopia.
Mkwasa ameeleza kuwa watafanya hivyo ikiwa ni sehemu ya kutia morali kwa wachezaji baada ya kazi nzito katika michuano ya Kombe la Shirikisho.
Tayari kikosi kwa ujumla kimesharejea nchini na sasa kitakuwa tayari kuanza maandalizi ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mbeya City FC.
Yanga imesonga mbele mpaka hatua ya makundi ya mashindano hayo kufuatia kuiondoa Dicha kwa idadi ya mabao 2-1.
Wajiandae kwa kipigo kizito kutoka kwa mnyama,tulieni tuli kwa mpira ule walioonyesha juzi kwa wahabeahi wajipange.
ReplyDeleteNaomba washauliwe hizo pesa siza kulipa madeni zimetoka kwaajili ya maandalizi ya timu kwaajiri ya hatua yamakundi.msije mkatuletea shida ya kufungiwa
ReplyDeletePili zinaitaji mrejesho siozinatoka kama pesa yanyanya nafikiri mlimsikia raisi washilikisho lampira duniani alieleza vizuri kabisa kuhusu pesa zinazo tolewa na mashirikisho
ReplyDelete