March 4, 2019

UONGOZI wa Ruvu Shooting umesema baada ya kuwashushia kichapo cha mabao 6-2 Mwadui FC sasa watakaofuata watapapaswa kama kawaida kwani tayari mbinu ya kocha imejibu.


Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amesema kwa sasa haoni mtu atakayewazuia, spidi yao ni kubwa mithili ya gari lililokata breki kwenye mteremko mkali.

"Kama gari kwa sasa tunasema limewaka na linapita kwenye mteremko mkali kuzuia huwa sio kazi rahisi, mbinu za mwalimu kujibu ni matokeo ya kupata ushindi kwa wapinzani wetu.

"Wachezaji wanatambua kazi yao na tayari akili zao zimejiweka sawa kwa ajili ya kuwapapasa Singida United na tutakuwa pale Namfua Singida Machi 7, mashabiki waendelee kutupa sapoti," amesema Bwire.

Ruvu Shooting wanaweka rekodi mpya mzunguko wa pili baada ya kufunga mabao mengi zaidi kwenye ligi msimu huu na pia mchezaji wao Fully Maganga aliepa na Mpira baada ya kupiga hat trick ya kwanza kwa Ruvu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic