March 6, 2019


Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu Tanzania Bara imemchagua Kocha wa Prisons ya Mbeya, Mohammed Rishard kuwa Kocha Bora wa mwezi Februari akiwashinda Kocha Mkuu wa Simba,  Patrick Aussems na Kocha Mkuu wa Mwadui, Ally Bizimungu. 

Rishard ameonesha mabadiliko makubwa kwa Prisons muda mfupi tu baada ya kukabidhiwa timu hiyo ambayo haikuwa ikifanya vizuri, lakini baada ya ujio wake aliiongoza Prisons kushinda michezo yote mitano iliyocheza na kupata pointi 15 ikipanda kutoka nafasi ya mwisho katika msimamo wa ligi hadi ya 14. 

Aussems yeye aliiongoza timu yake katika michezo mitano iliyocheza na kushinda yote ikivuna pointi 15 na kupanda kwa nafasi moja kutoka ya nne hadi ya tatu, wakati Bizimungu aliiongoza Mwadui kushinda michezo mitatu na kupoteza miwili ikipata pointi tisa na kupanda kwa nafasi mbili kutoka ya 17 hadi ya 15. 

TFF ina utaratibu wa kuwazadiwa wachezaji bora wa kila mwezi, huku pia mwisho wa msimu kukiwa na tuzo mbalimbali zinazohusu ligi hiyo, ambapo msimu wa mwaka 2017/2018  tuzo 16 zilitolewa kwa washindi wa kategori mbalimbali.

Washindi (Mchezaji na Kocha) kila mmoja atapata kitita cha sh. 1,000,000 (milioni moja) na tuzo (trophy) kutoka kwa wadhamini Biko Sports pamoja na kisimbusi kutoka kwa watangazaji rasmi wa TPL kampuni ya Azam TV.

4 COMMENTS:

  1. Nani kafunga magoli mengi zaidi na kaiongoza kucheza mechi takribani kila baada ya saa 72?Wanajifanya hawajui Aussens yupo?Angekuwa Zahera kashinda mechi nne mfululizo hapo angechaguliwa

    ReplyDelete
  2. Aussems kawafunga midomo ndo kocha bora mechi ngumu mwezi februari utatoboa yeye ndo ataibuka kidedea mwisho wa mwaka huu

    ReplyDelete
  3. Kwahyo mechi na Al ahly hamuijui TFF???? 😨😨😨

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic