UKANDA wa Afrika Mashariki kwa sasa Simba ndiyo timu kubwa ambayo imefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa ambayo ni mikubwa Afrika.
Simba wametinga hatua ya robo fainali baada ya kutumia vema Uwanja wa nyumbani katika michezo mitatu waliyocheza ambapo hawajaruhusu kufungwa zaidi ya kuruhusu bao moja tu ila pointi zote tisa wamebebea Uwanja wa Taifa.
Ugenini Simba haijafunga bao hata moja zaidi imefungwa jumla ya mabao 12 na jumla imefungwa mabao 13 ikiwa ni timu ambayo imefungwa mabao mengi zaidi.
Hawatakutana na waarabu Al Ahly kwenye hatua ya robo fainali kwani wote walikuwa kundi D, rekodi zinaonyesha kuwa mwaka 1974 walitinga hatua ya nusu fainali.
Timu ambazo zimefuzu hatua ya robo fainali ambazo leo zitatambua mbaya wao ni pamoja na Wydad Casablanca, Mamelod Sundowns, Esperance, Horoya Athletic Club, TP Mazembe, CS Constatine, Al Ahhly na Simba.
0 COMMENTS:
Post a Comment