Kocha Talib Hilal ambaye ni Mtanzania amefanikiwa kuipeleka timu ya Taifa ya soka la Ufukweni ya Oman kushiriki kombe la Dunia nchini Paraguay.
Hii na mara ya tatu Hilal anafanikiwa kuipeleka Oman kushiriki mashindano makubwa kwenye soka la ufukweni.
Hilal aliwahi kuichezea na kuifundisha timu ya Simba ambayo kwa sasa imetinga hatua ya robo fainali Afrika baada ya miaka 16 kukatika, pia aliwahi kuchezea timu ya Taifa.
Michuaono hii itafanyika mwaka huu kwenye mji wa Asucion kuanzia November 21 mpaka December 1.
0 COMMENTS:
Post a Comment