March 20, 2019


Kamati Maalumu ya Yanga imekubaliana kutoa kwa Awamu Mrejesho wa Mpango Mkakati uliozingatia kwa wanachama na Wapenzi wa Yanga ili kujenga uelewa miongoni mwao ili kufikia Malengo Kusudiwa.

Yanga kwa sasa wanapitia changamoto ya mpito hasa kutokana na kujiendesha kwa kutegemea nguvu za wananchi na michango yao.

Kwasababu hiyo Klabu ya Yanga kwa kushirikiana na Wadau Mbalimbali chini ya Uratibu wa Kocha Mwinyi Zahera wamebuni njia bora na endelevu ya kuweza kupata pesa kwa haraka na kuweka mfumo bora wa kuendeleza kitakachopatikana.

Kupitia ushirikiano huo ambao uliratibiwa vyema na Wachezaji pamoja na Benchi la Ufundi, wamefungua Akaunti ya Kukusanyia fedha i nayoitwa YANGA COLLECTION A/C No: 0150419775800 CRDB BANK - VIJANA BRANCH ili wapenzi na wanachama wa Yanga waweze kuchangia timu yao. 


Katika kuboresha wazo hilo Uongozi wa Yanga uliunda Kamati Maalumu ya Kuhamasisha Uchangiaji 09/03/2019 ili ibuni na kuweka Mikakati madhubuti kufanikisha zoezi hili ndani ya muda mchache ili Klabu ya iweze kujikwamua kiuchumi.

 Kazi ya kamati hiyo ni kama ifuatavyo:-

i) Kuandaa Mpango Kazi wa kufanikisha zoezi hili la uchangiaji kwenye Klabu ya Yanga kwa muda mfupi, Kati na Mrefu.

ii) Kuandaa Mkakati maalumu wa namna nzuri ya kukusanya pesa kwa watu ambao wana mapenzi na Yanga bila kujali rika, jinsia na maumbile yao.

iii) Kuboresha Mkakati uliopo sasa wa ukusanyaji pesa pamoja na kuandaa mpango wa utunzaji wa pesa zitakazo kusanywa pamoja na mrejesho kwa wachangiaji.

iv) Kuzindua rasmi mpango wa uchangiaji ili uweze kuleta tija na kufikia malengo yaliyokusudiwa.

v) Kuushauri uongozi wa Yanga juu ya njia sahihi na bora zaidi kwa siku za usoni ili kuwa na Yanga imara.

6 COMMENTS:

  1. Mpango wa hakika na bora ni ule wa timu kujipatia pesa za hakika na zakuendeleo sio kutegemea kwa kila kitu na siku zote pesa za bakuli kwasababu michango ina kikomo chake na hali zinajulikana
    kuzungusha bakuli ambazo

    ReplyDelete
  2. Hilo ni wazo zuri, lakini pia kama klabu inatakiwa kuazisha vyanzo vingine vya mapato ikiachana na michango ya wadau wa yanga.

    ReplyDelete
  3. Wazo lingine uchaguzi ndani ya klabu hiyo kwa sasa ni muhimu sana kuliko wakati mwingine wowote.

    ReplyDelete
  4. Huo mpango mi navyoona ungeelekezwa katika kuongeza wanachama marudufu hata laki moja tu. Wakichangia ada za uanachama kwa mwaka kila kichwa hata 12000/= timu itakuwa na nguvu ukijumlisha na viingilio na wadhamini

    ReplyDelete
  5. Huo mpango mi navyoona ungeelekezwa katika kuongeza wanachama marudufu hata laki moja tu. Wakichangia ada za uanachama kwa mwaka kila kichwa hata 12000/= timu itakuwa na nguvu ukijumlisha na viingilio na wadhamini

    ReplyDelete
  6. Huo mpango mi navyoona ungeelekezwa katika kuongeza wanachama marudufu hata laki moja tu. Wakichangia ada za uanachama kwa mwaka kila kichwa hata 12000/= timu itakuwa na nguvu ukijumlisha na viingilio na wadhamini

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic