March 28, 2019


Imeelezwa kuwa Singida United imejutia kusajili nyota wanaotoka klabu za Simba na Yanga wakidai wao ndio chanzo cha migogoro ndani ya timu yao.

Chanzo kimeeleza Singida United wamekuwa na msimu mbaya mwaka huu wa kushika nafasi ya tatu kutoka mkiani kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, wakiwa na pointi 33 wakicheza michezo 30.

Taarifa imeeleza Mkurugenzi wa Singida United, Festo Sanga, alisema kufanya vibaya kwa timu hiyo kumetokana na kusajili wachezaji wengi kwa gharama kubwa.

Sanga amesema gharama hizo zimewafanya kushindwa kumudu matumizi na kujikuta wakijiendesha kwa tabu.

1 COMMENTS:

  1. Mficha maradhi siku zote kifo hakiwachi kumnyembelea kwani tatizo halisi la Singida United ni la wao wenyewe singida na kamwe haliwezi kuwa la wachezaji wanaotoka timu fulani. Kufeli kwa Singida kumechangiwa na baadhi ya viongozi timu hiyo kuitambulisha singida united kama kikosi cha Yanga B na sio timu inayowakilisha mkoa wa singida. Hata Mohamedi Mo wa Simba anatokea Singida na kuna wadau wengine wengi maarufu na wenye nguvu ya hali na mali na isingekuwa shida kuipiga tafu Singida United kama kweli ingekuwa timu yenye kuweka usingida mbele kuliko uyanga mbele.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic