STRAIKA MTAMBO SIMBA WAPELEKA HOFU MAZEMBE
Straika mapafu ya mbwa katika kikosi cha Simba, Mrwanda, Meddie Kagere, amesema hana hofu na TP Mazembe katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
Kagere ambaye ameshajihakikishia namba katika kikosi cha kwanza, ameeleza kila hatua wanayofikia wanajipanga vilivyo ili kupata matokeo.
Simba baada ya kuingia hatua ya robo fainali walipangwa na Mazembe iliyotinga pia hatua hiyo na mechi yao ya kwanza itachezwa April 5-6 mwaka huu ambapo Simba wataanzia Dar.
"Sina hofu yoyote kuelekea mechi hiyo.
"Kikubwa ni maandalizi na tunaendelea kujiandaa. Tutapambana kadri ya uwezo wetu kuhakikisha tunapata ushindi.








Sikioni Simba cha kukihofia kutoka kwa MAZEMBE.Kweli ni timu yenye uzoefu kwenye mashindano makubwa Africa. Ila kwa Simba ni nafasi nyengine muhimu ya kujua ubora na mapungufu yao kama timu. Simba wanatakiwa kusahihisha madhaifu yao wanapocheza mechi za ugenini. Suala hili linatakiwa kutawala mjadala katika kuhakikisha Simba wanavuka hatua ya robo fainali. Mazembe walishajua kuwa kupata matokeo mbele ya Simba Daresalaam ni kitu kigumu kwa hivyo watakuja na mbinu mbadala za kuikabili Simba nje na ndani ya uwanja kwa hivyo Simba wanatakiwa kuwa makini muda wote mpaka mechi zao na Mazembe zinakamilika. suala la kujiuliza timu yenye mabeki wagumu kama Juuko,wawa,Bukaba,kwasi,
ReplyDeleteNyoni,kulibali,Mlipili vipi inashindwakuwa na beki imara? Moja katika yote nadhani uongozi wa Simba wanapaswa kumshauri kocha wao mkuu kuongeza kocha wa mabeki katika benchi lake la ufundi ili kutengeneza Simba imara zaidi.