March 9, 2019


KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa kwa sasa kikosi chake kipo kamili gado kuvaana na KMC kesho mchezo wa Ligi Kuu Bara, Uwanja wa Taifa.

Mchezo wa  mzunguko wa kwanza Yanga ilisepa na pointi tatu dakika za lala salama baada ya Feisalim Abdalah 'Fei Toto' kupachika bao dakika ya 89.

Zahera amesema anatambua ushindani ulivyo na namna timu nyingi zinavyokamia kuifunga Yanga ila hilo ni gumu kutokea kwa sasa.

"Tunakaza mwanzo mwisho, hakuna ambaye atatuangusha, nimewasoma wapinzani wangu kupitaia kanda zao za video sasa kazi ni moja tu ushindi," amesema Zahera.

Kocha wa KMC, Ettiene Ndiyaragije amesema anatambua ugumu uliopo kwenye mchezo wake wa kesho ila amewapa mbinu wachezaji wake kupata matokeo.

"Ushindani ni mkubwa na kila timu inahitaji matokeo, nimewapa mbinu wachezaji wangu ili kuona tunabeba pointi tatu," amesema Ndiyaragije.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic