March 28, 2019


Kikosi cha Yanga kimewasili salama jijini Mwanza kwa ajili ya mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Alliance Schools.

Yanga itakuwa na kibarua dhidi ya Alliance ambao maskani yao ni ndani ya jiji hilo utakaopigwa Jumamosi ya wiki hii.

Kuelekea mchezo huo, Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera, amemuondoa Ajibu kwenye kikosi kutokana na kutokuwa fiti kiafya.

Ajibu amekuwa akisumbuliwa na nyama za paja na kwa mujibu wa Zahera ameeleza hawezi kuwa sehemu ya mchezo huo Jumamosi.

Mshindi wa mechi hiyo atatinga moja kwa moja hatua ya nusu fanali ambapo timu zilizofika hatua hiyo ni Lipuli na KMC FC.

4 COMMENTS:

  1. Hapo sawa kumbe ni tatizo la nyama za paja, nilidhani kutokana na habari ile kuwa anarejea nyumbani kumenoga!

    ReplyDelete
  2. Ajibu sio mgonjwa na yuko fiti 150% ila ndo kama ulivyoskia kalejea home

    ReplyDelete
  3. Au huenda ikawa hawamuamini tena kwakuwa hatokuwa na morali ya kuichezea timu yake yumo njiani kurejea nyumbani alikozaliwa na kulelewa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic