March 30, 2019


KOCHA Mkuu wa Yanga, Mkongoni, Mwinyi Zahera ameamua kuvunja ukimya baada ya kusema mchezaji yeyote ambaye anataka kuondoka ndani ya kikosi hicho ni ruksa.

Kwa sasa kumekuwa na tetesi za mastaa kibao wa timu hiyo wakihusishwa na timu nyingine kama Ibrahim Ajibu, Kelvin Yondani na Papy Kabamba Tshishimbi ambao wanaripotiwa kutakiwa na Simba.

Kutokana na tetesi hizo, Kocha Zahera alisema kuwa, haogopi kusikia mchezaji fulani anaondoka kwenye kikosi chake kwa sababu kuna wakati wachezaji hao ambao wanatajwa kuondoka wanakuwa hawapo kwenye timu na bado wamekuwa wakipata matokeo.

Kocha huyo alisema amekuwa akipigiwa simu na mashabiki ambao wamekuwa wakihoji kuwa wamekuwa wakisikia wachezaji Tshishimbi, Feisal Salum ‘Fei Toto’ na Yondani lakini yeye amekuwa akiwaambia wasijali mambo yatakwenda sawa hata kama wataondoka.

Zahera aliongeza kuwa tayari ameshawaambia viongozi wa timu hiyo kuwa hawapaswi kutetemeka wala kuwa na hofu kisa tu mchezaji fulani anaondoka klabuni hapo kwani kuna baadhi ya mechi wamekuwa wakishinda bila wao kucheza.

“Hakuna mchezaji yeyote anayeweza kuzuiwa kuondoka ndani ya Yanga na timu ikayumba hilo halipo na haliwezi kuniogopesha na mchezaji ambaye anataka kuondoka ndani ya klabu ruksa kwenda na Yanga itabaki kuwa bora.

“Nimejipanga kuhakikisha namaliza usajili wa wachezaji wangu mbele ya Mei 15, mwaka huu
kabla ya Juni Mosi ambapo itakuwa na majukumu ya timu ya taifa ya DR Congo huko Ulaya,” alisema Zahera.

3 COMMENTS:

  1. Bora upunguze jazba bwana Zahera kwasababu hatuwa na matamshikama hay o yatawafanya hao wapya unaowataka kuwasajili wajihisi kutokuwa katika amani katika kikosi chako na uzijuwe sababu aa idadi kubwa za wachezaji nyota wanaotaka kuondoka na kuzifanyia kazi

    ReplyDelete
  2. Kweli kabisa kwasababu nyumba uliyoijenga kwa muda wa mwaka mmoja waweza kuibomoa kwa siku moja tu na jee kutokana na hali ya kifedha ya timu ya sasa inayo uwezo wa kuwanunua upya mastaa wenye uwezo kama hao uliowafungulia milango ya kutokea?

    ReplyDelete
  3. Hapo KWELI yanga WAMEMPATA kocha KICHAA MWENYE HELA AHAHAHAA

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic