April 24, 2019


Kinda wa Serengeti Boys na mchezaji wa Singida United kabla hajatimkia MFK Czech na baadae kwenda Minnesota Fc nchini Marekani, Ally Hamis Ng'anzi anaendelea vizuri kusakata kabumbu nchini humo akitafuta njia ya kucheza soka kwenye ligi kubwa zaidi huko ughaibuni, kwa mujibu wa uongozi wa Singida United kupitia Mkurugezi Mtendaji, Festo Sanga.

Ally Ng'anzi anayecheza nafasi ya kiungo (holding Mid) anasema ndoto zake ni kufika mbali, anaitumia nafasi hiyo ya kucheza MLS kama kete mhimu maishani mwake kukua kisoka ili afike mbali zaidi.

N'gazi pia ni moja ya mafanikio ya PROJECT (mradi) ya kutoa nafasi kwa wachezaji kwenda kusakata soka ndani na nje ya Africa.

Tunawashukuru wadau wote ambao wanashiriki kwenye kuwezesha hili, Nizar Khalfan, Ibrahim Mohamed, TFF kwa jitihada zenu kufanikisha safari za vijana hawa.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic