April 24, 2019


Tetesi za soka barani ulaya leo Jumatano

City waingiwa na hofu kwa Sane

Manchester City wana hofu kuwa winga wao Mjerumani Leroy Sane mwenye umri wa miaka 23 anaagalia uwezekano wa kuondoka kwenye klabu hiyo kutokana na kwamba mazungumzo ya mkataba wake yamekwama (Metro)

Man United yamchagua Trippier kuwa mbadala wa Bissaka

Manchester United wamemchagua mchezaji wa timu ya Uingereza ya Tottenham Kieran Trippier mwenye umri wa miaka 28 kama mchezaji mbadala wanayemlenga kumchukua ikiwa watashindwa kusaini mkataba na Aaron Wan-Bissaka, mwenye umri wa miaka 21 kutoka Crystal Palace. (Mirror)

Kwa upande mwingine United wanaamini Mbeljgiji Thomas Meunier mwenye umri wa miaka 27 anayechezea Paris St-Germain kama beki wa kulia ni mchezaji ambaye anayeweza kupatikana kwa bei nafuu na kwa urahisi anayeweza kujaza nafasi ya Trippier au Wan-Bissaka. (Independent)

Liverpool yaingia vitani na Atletico kwa Grujic

Liverpool watadai euro milioni 40 kwa Mserbia Marko Grujic mwenye umri wa miaka 23 ambaye ni kiungo mshambuliaji huku klabu ya Atletico Madrid ikionyesha pia nia ya kumtaka. (ESPN)

Imeelezwa pia Liverpool watataka malipo ya 40m euros kwa Mserbia Marko Grujic

Newcastle yaanza kumsaka mbadala wa Benitez

Newcastle wanaangalia uwezekano wa kumchukua meneja wa AC Milan Mtaliano Gennaro Gattuso kuchukua nafasi ya kocha wao Rafael Benitez ikiwa ataamua kuondoka mwishoni mwa msimu huu. (Gazzetta - in Italian)

Mshambuliaji wa Manchester City Riyad Mahrez anatishia kuondoka kwenye klabu hiyo, winga huyo Mualgeria amekuwa akilalamika wazi juu ya kunyimwa muda wa kucheza chini ya Kocha Pep Guardiola. (Mail)

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic