Kiujumla kikosi cha jana cha Simba kinahitaji pongezi, wachezaji wamecheza mechi kwa kujituma kwelikweli. Hakika hii inaleta sasa maana ya kikosi kipana.
Pia, kuna wzchezaji wamebadilika kabisa uchezaji wao, yaani wameongeza kujiamini na pia wameongeza stamina katika uchezaji, na vilevile wameongeza kiwango cha kumudu kukaba, sio kama zamani ambavyo walikuwa wakikabia macho, wakipoteza mpira wanatembea uwanjani; mfano wa wachezaji hao ni kama vile Nickoras Gyan, Asante Kwasi, Mlipili, Salamba, wachezaji hawa wameongeza kitu katika uchezaji wao, jana wamenifurahisha sana, kwani wamepelekea timu kucheza kwa kujituma sana mwanzo hadi mwisho kwa kuungana na wenzao ambao huanza mara nyingi kikosi cha kwanza ambao uchezaji wao ulishakuwa wa kujituma tangu mechi za kimataifa, hivyo ikafanya mzani wa timu uwe kati.
Ushauri wangu mwingine kwa kocha ni kuhusu Mchezaji Mkude, kwakweli huyu jamaa kwasasa angepewa mazoezi maalumu kwanza ili aendane na kasi ya kikosi ya kwanza.
Kwasababu ubora wake ule ambao binafsi naufahamu sio huu alionao, kiukweli ameporomoka, na sijui ni nini sababu, kwasababu namba ya kikosi cha kwanza anaipata kila mechi ukiondoa hii ya jana, lakini ni nini ambacho kinamfanya ashindwe kujiamini! Mimi naona kazi yake uwanjani kwasasa ni kukimbia-kimbia tu uwanjani. Kukaba hakabi, akipewa pasi nzuri na wenzake yeye anapoteza mpira au akifanikiwa kutoa pasi basi unakuta pasi hiyo haifiki kwa mlengwa.
Naomba kocha amuandalie program maalumu na namba ya kikosi cha kwanza amuachie mchezaji mwingine kwani namba yake hata Haruna anaimudu, Kotei anaitendea haki, kiujumla Simba kuna viungo wengi sana. Apumzike kidogo ili arudishe utimamu wake. Maana baada ya skendo yake ya kutoroka kambini kwenda klabu, ndo kiwango kimeporomoka kabisa!
Shukuruni kwasababu nusu ya kikosi cha Simba ni kikosi cha akiba
ReplyDeletewacheni kiendelee kucheza kina usongo wa benchi
ReplyDeleteKiujumla kikosi cha jana cha Simba kinahitaji pongezi, wachezaji wamecheza mechi kwa kujituma kwelikweli. Hakika hii inaleta sasa maana ya kikosi kipana.
ReplyDeletePia, kuna wzchezaji wamebadilika kabisa uchezaji wao, yaani wameongeza kujiamini na pia wameongeza stamina katika uchezaji, na vilevile wameongeza kiwango cha kumudu kukaba, sio kama zamani ambavyo walikuwa wakikabia macho, wakipoteza mpira wanatembea uwanjani; mfano wa wachezaji hao ni kama vile Nickoras Gyan, Asante Kwasi, Mlipili, Salamba, wachezaji hawa wameongeza kitu katika uchezaji wao, jana wamenifurahisha sana, kwani wamepelekea timu kucheza kwa kujituma sana mwanzo hadi mwisho kwa kuungana na wenzao ambao huanza mara nyingi kikosi cha kwanza ambao uchezaji wao ulishakuwa wa kujituma tangu mechi za kimataifa, hivyo ikafanya mzani wa timu uwe kati.