April 6, 2019


BAADA ya kikosi cha Azam FC kuibuka na ushindi mbele ya Kagera Sugar, tayari kikosi kimeanza kujiandaa kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mbao FC.

Mchezo huo utachezwa kesho Uwanja wa CCM Kirumba mkoani Mwanza  majira ya saa 10:00 jioni.

 Mtaribu wa Azam FC, Philip Alando amesema kuwa kikosi kipo tayari kwa ushindani na hesabu kubwa ni kupata pointi tatu na morali ni kubwa kwa kila mchezaji.

"Vijana wana morali kubwa na wapo tayari kwa ushindani kikubwa ni sapoti ya mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanjani na kuona namna soka litakavyochezwa kwani ligi ina ushindani mkubwa kwa sasa," amesema Alando.

 Mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Chamazi Azam iliibuka na ushindi wa mabao 4-0.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic