YANGA YATIA TIMU MWANZA, SASA KUIVAA LYON BAADA ya kugawana pointi moja na kikosi cha Ndanda mkoani Mtwara kwa kufungana bao 1-1, leo kikosi cha Yanga kimetia timu Mkoani Mwanza. Yanga itacheza na African Lyon siku ya Jumatatu Uwanja wa CCM Kirumba. Mchezo wa kwanza waliocheza na Lyon Yanga iliibuka kidedea na ushindi wa bao 1-0 Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
0 COMMENTS:
Post a Comment