April 15, 2019


Aliyewahi kuwa mchezaji wa zamani wa Yanga na sasa ni mchambuzi mwandamizi, Ally Mayay Tembele, ameshauri viongozi wa wapya wa klabu hiyo watakaopatikana wafanye sensa ili kujua klabu ina watu wapi nyuma ya Yanga. Imeelezwa.

Taarifa imeeleza kuwa Mayay ambaye aliichezea Yanga kwa mafanikio ameshauri jambo hilo kufanyika kutokana na ukubwa wa klabu hiyo ambayo ina zaidi ya miaka 80 sasa.

Mayay ameeleza kuwa kufanyika kwa sensa hiyo kutasaidia kuijua vizuri thamani ya Yanga akisema kuwa thamani ya kitu ni watu.

Mbali na ushauri huo, Mayay pia amewataka viongozi wapya watakaopatikana baada ya uchaguzi waige kufanya mabadiliko ya uendeshwaji wa klabu kwani kuiga si dhambi.

Klabu hiyo inaenda kufanya uchaguzi wake mkuu Mei 5 mwaka huu ili kupata viongozi wake wapya watakaoingoza kwa miaka minne ijayo.


1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic