KOCHA wa Biashara United, Amri Said amesema kuwa anachukizwa na nafasi ya 19 aliyopo kwa sasa akiwa na pointi 34, amepania kushinda mechi zake zote walizobakiza kwa sasa kwenye ligi kwa hasira.
Biashara United imecheza michezo 31 kwenye ligi na imebakiza michezo saba ili kutimiza mzunguko wa pili ambapo kama itashinda yote itajikusanyia pointi 21 na kufikisha pointi 55 zitakazombakiza kwenye ligi.
Said amesema kuwa ana imani kikosi chake hakitashuka daraja msimu huu kwa kuwa tayari amewajenga kisaikolojia wachezaji wake licha ya kupitia kwenye ukata.
"Hatupo kwenye nafasi nzuri kwa sasa, hilo lipo wazi ila dawa yake nimeshaigundua ni kushinda mechi zote zilizopo mkononi mwangu na hilo ni jambo linalowezekana kwa kuwa tuna nia.
"Vijana wangu wana nguvu na uwezo mkubwa wa kupambana hivyo kwa sasa kila tutakayemfuata ama atakayetufuata ajiandae kuacha pointi tatu hatuna cha msalie mtume mida mibovu hii kwa sasa," amesema Said.
0 COMMENTS:
Post a Comment