KOCHA Mkuu wa Simba amesema kuwa licha ya kuwakosa nyota wake wawili kwenye safu ya ulinzi bado ana imani ya kufanya vizuri kwenye mchezo wa leo wa ligi kuu dhidi ya Alliance ya Mwanza utakaopigwa uwanja wa CCM Kirumba.
Aussems amesema kuwa leo atawakosa wachezaji wake wa kikosi cha kwanza ambao ni beki Pascal Wawa na Erasto Nyoni kutokana na kutokuwa sawa kiafya hali ambayo imemfanya abadili kikosi kitakachoanza leo.
"Natambua leo nitawakosa Nyoni na Wawa ila hilo halinipi taabu kwa kuwa tayari nimewapanga Mlipili na Paul Bukaba ambao nipo nao muda mwingi kwenye mazoezi hali ambayo inanifanya nijiamini.
"Mchezo wa leo ni mgumu kwa kuwa napambana na timu ambayo inapambana kubaki ligi kuu, pia nami nipo kwenye mbio za kutwaa ubingwa nadhani unaona ni namna gani ushindani utakuwa mkubwa," amesema Aussems.
0 COMMENTS:
Post a Comment