April 12, 2019


Kamati ya Hamasa ya Kuchangia Klabu ya Yanga inatoa shukurani kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Majaliwa Kassim Majaliwa kwa kuwa mchangiaji wa kwanza kuichangia Klabu ya Yanga.

Majaliwa ameichangia Yanga ambayo ina historia kubwa ya upatikanaji wa Uhuru wa Nchi yetu ya Tanzania. 

Waziri Mkuu ameichangia Klabu ya Yanga kiasi cha shilingi milioni moja *(1,000,000/=)*. 

Kamati ya Hamasa kwa niaba ya Wanachama, Mashabiki na Wapenzi wa Klabu ya Yanga ina imani kubwa kuwa, mchango huu utakuwa chachu kwa Viongozi wengine wa ngazi zote kwa Taasisi za Umma na Binafsi bila kujali Itikadi, Jinsia na hata Ushabiki wa kijadi wa Yanga na Simba na hatimaye kuunga mkono jitihada hizi za Kiukombozi za *KLABU YA YANGA* zenye kauli mbiu ya *Timu ya Wananchi Wawekezaji ni Wananchi Wenyewe*

Cheti Maalumu kitatolewa kwa Mh. Waziri Mkuu na Mwenyekiti wa Kamati *Mh. Anthony Peter Mavunde (MB)* wakati wa kuhitimisha zoezi hili Maalumu *Deo Mutta*
*KNY - Kamati ya Hamasa ya Kuchangia

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic