YONDANI KUKOSA MECHI TATU LIGI KUU NA FAINI YA LAKO TANO
Beki kisiki wa Young Africans Kelvin Yondani sasa atakosa jumla ya mechi tatu zijazo katika ligi
Adhabu hiyo atakubana nayo kufuatia kupewa kadi nyekundu ya moja kwa moja kwenye mchezo wa jana dhidi ya Kagera sugar uliomalizika kwa Yanga kushinda mabao 3-2.
Beki huyo atakosa mechi hizo kwa kosa la kupiga kiwiko mchezaji wa Kagera na kupelekea kulimwa kadi hiyo.
Kwa mujibu wa kanuni za wanaoendesha mpira, Yondani atakosa michezo mitatu mfululizo ya Yanga SC ama kupigwa faini sh.500,000.
Michezo mitatu atakayoikosa beki huyo kisiki nchini ni dhidi wakata miwa wa Mtibwa Sugar ambao utachezwa Morogoro (17 April 2019) Azam FC vs Yanga (29 April 2019) na Mchezo wa FA dhidi ya Lipuli FC utakaopigwa Iringa.
Vita hii ya (TFF, Bodi ya Ligi na Waamuzi) dhidi ya Yanga itashindwa tu....Mungu yuko upande wa Yanga
ReplyDeleteMcheze rafu mpepewe na kanga?
ReplyDeleteAI kwahiyo ulitaka apige wenzake viwiko na awatemee mate then aachwe tu si ndio, acha ulimbukeni, huo ushabiki wa kizamani sana, chezeni mpira bhana...au kwa vile mlishazoea mbeleko ndio maana, sambusa weeeeee.......
ReplyDeleteAl mchango wako unaheshimika hapa.Unapoanza kuandika kishabiki unatutoa imani.Nyondani kämpiga mtu kiwiko na kwa mujibu wa sheria za mpira lazima apewe kadi nyekundu. Kufungiwa mechi 3 na faini ni kanuni kwa kila mchezaji bila kujali anataka timu upp.Bocco alifungiwa mechi 3,Kotei alifungiwa mechi 3.Kuwa mkweli usiyumbishwe nä ushabiki.
ReplyDeleteSafi kabisa....mwaka Jana alitemea mate mchezaji simba!hakuna adhabu.wasiwasi wao tu!kama una bahati utashinda kwa bahati tu mwanzo mwishi hats TFF wakiweka figisu za ratiba!
ReplyDeleteLipuli anaisubiri Yanga bila Ajibu na Yondani
ReplyDelete