April 30, 2019





Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limeipitisha Simba kuwavaa moja ya vigogo wa Ulaya, Sevilla Mei 23 jijini Dar es Salaam.

Sevilla ni moja ya kikosi bora barani Ulaya kutoka nchini Hispania na kinatarajia kuwa na ziara nchini, mwishoni mwa Mei.

Habari kutoka ndani ya TFF, zimeeleza kuwa shirikisho hilo limetoa nafasi kwa Simba kutokana na kuwa mabingwa watetezi lakini waliokuwa wawakilishi wa Tanzania waliofika robo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Sevilla inaletwa nchii na wadhamini wakuu wa Simbana Yanga, kampuni ya kubeti ya SportPesa ambayo sasa ni kampuni maarufu zaidi ya michezo hiyo nchini.

3 COMMENTS:

  1. Safi Kabisa Tff Wameangalia Vigezo Na Si Ushabiki Simba Mjitume Huenda Wachezaji Wetu Wakapata Fursa Hiyo Ikaleta Faida Aidha Kwa Nchi Au Club

    ReplyDelete
  2. Ila kama Yanga tayari walishaanza usajili tena kwa wachezaji wa kigeni nitashangaa sana kwa Simba kama hawatatumia mechi hii ili kujiridhisha na wachezaji wanaotaka kuwasajili kwa ajili ya mashindano mbalimbali mwakani. Sio siri kwa Simba kumekuwa na kasi ndogo isiendana na mahitaji ya timu katika suala la usajili.Vipigo vya aibu Klabu bingwa Africa hahuhitaji mtaalam wa usajili kufahamu yakuwa Simba ni weupe kunako eneo la ulinzi wanapokutana na tumu kubwa yenye ushindani wa kweli kwa hivyo suala la kuimarisha backline ya Simba lilikuwa ni ombi la kocha wa Nkana red devils ya Zambia zamani tu lakini mpaka leo hakuna kilichofanyika. Timu ina wachezaji wazuri na wenye kujituma ila maboresho lazima tena ya haraka ili wachezaji wapate kuzoweana sio kusubiri mpaka mashindano yanaanza ndio kuhangaika na usajili.kiufasaha kabisa Simba inahitaji kiungo wa ulinzi na wa ushambuliaji wa ziada wenye kasi zaidi. Na nyongeza ya fowadi mwenye kasi ya utupiaji zaidi. Kama uwezo upo basi Simba wanapaswa kumfuatilia fowadi tishio wa Nkana Idris Mbombo aliehamia moja ya klabu za sudani elhilali kama sikosei.Yule kijana ni balaa. Simba wanaweza kutumia hii hali ya sintofahamu ya kisiasa sudani kumshawishi na kumleta Tanzania.Hapana shaka ni miongoni mwa wachezaji ghali katika ukanda wetu huu lakini shughuli yake uwanjani ni pevu kweli kweli vile vile.

    ReplyDelete
  3. aya tuzione hamsa+hamsa zingne siku hyo.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic