LEO Julai 22 Ligi Kuu Tanzania Bara inaendelea ambapo vita ni kubwa kwenye upande wa kusaka nafasi ya kubaki ndani ya Ligi Kuu Bara.
Timu 10 zitakuwa uwanjani kusaka pointi tatu kwenye viwanja tofauti na hesabu zao zipo namna hii:-
Mbao v
Namungo, Uwanja wa Kirumba( Mbao ipo nafasi ya 19 ina pointi 39 inakutana na Namungo ina pointi 64 nafasi ya nne).
Safu ya
ushambuliaji ya Mbao imefunga jumla ya mabao 28, kinara ni Wazir Jr ana mabao
12/ Namungo safu yao ya ushambuliaji imefunga mabao 44 kinara wao ni Relliants
Lusajo ana mabao 12.
Mbao inasaka
nafasi ya kubaki ndani ya Ligi Namungo haina cha kupoteza ila inawania nafasi
ya pili kimyakimya.
Singida
United v Kagera Sugar, Liti( Singida United ina uhakika wa kushiriki Ligi
Daraja la kwanza ina pointi 18 baada ya kucheza mechi 36/ Kagera Sugar wana
uhakika wa kubaki ndani ya ligi, ipo nafasi ya 8 pointi 49.
Mwadui v
Biashara United, Karume/Fainali ya kusaka nafasi ya kubaki ndani ya ligi, Mwadui FC ipo nafasi ya 15 pointi 41/ Biashara
United nafasi ya 9 pointi 47 ikipoteza mechi mbili inakwenda na maji.
Mtibwa v
Yanga, Jamhuri/ Mtibwa ipo nafasi ya 14 pointi 41 inavutwa shati na Lipuli ipo
nafasi ya 17,Mwadui ipo nafasi ya 15, Alliance nafasi ya 16 zote pointi 41./
Yanga inapambania nafasi ya pili ikiwa nafasi ya pili na pointi 68 inavutwa
shati na Azam FC yenye pointi 66 ikiwa nafasi ya tatu.
Safu ya
ushambuliaji ya Mtibwa Sugar imefunga mabao 27/ Yanga mabao 43. Pande wa safu ya ulinzi
Mtibwa imefungwa mabao 32/Yanga 27
KMC v
Tanzania Prisons, Complex/ zote mbili hazina uhakika wa kubaki ndani ya ligi, KMC
ipo nafasi ya 11 pointi 46/ Prisons ipo nafasi ya 12 ina pointi 45 ambazo
zinaweza kufikiwa na Mbao FC
0 COMMENTS:
Post a Comment