April 10, 2019


KIUNGO mpaka rangi wa Simba, Clatous Chama raia wa Zambia, amehuzunika kwa kushindwa kuwafunga TP Mazembe kwenye Dimba la Taifa lakini akaweka wazi kwamba hukohuko kwao DR Congo watafungika.

Mzambia huyo juzi Jumamosi alikuwa mmoja wa viungo walioanza katika kikosi cha Simba katika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya TP Mazembe. Mechi hiyo ilimalizika kwa suluhu.

Timu hizi mbili zitarudiana Aprili 13, katika mechi ya pili itakayopigwa Lubumbashi, DR Congo kuamua timu itakayofuzu nusu fainali.

Kiungo huyo mwenye miaka 27 amesema kuwa matokeo hayo kwao hayakuwa bora sana lakini watapambana katika mechi ya Congo ili wapate ushindi.

“ H a t u k u w a tunataka mechi hii imalizike kwa matokeo ya namna hii. Lakini kuna nafasi ya pili tutafanya kile kitu ambacho t u m e s h i n d w a kukifanya hapa Dar,” alisema Chama mwenye mabao matano katika Ligi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic