April 10, 2019


Kamati ya Uchaguzi ya Yanga na ile ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) zimefanya mchujo wa awali kwa wagombea katika uchaguzi wa klabu ya Yanga huku Dk Mshindo Msola, Lucas Mashauri na Elias Mwanjala wakipenya kuwania nafasi ya kumrithi Yusuf Manji. 



Wagombea waliopitishwa ni Dk Mshindo Msola, Lucas Mashauri na Elias Mwanjala wanaogombea nafasi ya Mwenyekiti. 


Wakati Janeth Mbena, katibu mkuu wa zamani wa TFF, Fredrick Mwakalebela, Thobias Lingalangala na Samwel Lukumay wanaogombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti. 

Wakati wagombea wa nafasi ya wajumbe ni Ally Sultan, Saad Khimji, Hassan Hussein, Siza Lyimo, Dominick Albinus, Seko Kingo, Hamad Islam, Shafiru Makosa, Injinia Leonard Marango, Cyprian Musiba na Injiani Bahati Mwaseba.

 Wengine ni Nassor Matuzya, Abdallah Chikawe, Hussein Nyika, Rodger Gumbo, Said Ntimizi, Palina Conrad, Elius Mkumbo, Suma Mwaitenda, Seif Hassan na Haruna Batenga.

4 COMMENTS:

  1. Do msolla, mwakalebela musiba naiona yanga ya kimataifa. Mirathi fc jiandaeni kisaikolojia hatuna masihara Safari hi. Hiyo ndo yanga bhana

    ReplyDelete
  2. Katika hao uliowataja mi namuona kiongozi wa soka mwenyewe weredi ni Mwakalebela

    ReplyDelete
  3. Huenda wakawatoa kwenye umatonya

    ReplyDelete
  4. Musiba Big No,labda Kama tunataka malumbano

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic