BEKI Kisiki wa Simba, Pascal Wawa amesema kuwa anawachukia wezi wa Bongo kutokana na kumfanyia kitu kibaya nyumbani kwake kwa kukomba kila kitu katika nyumba anayoishi maeneo ya Kunduchi na amesema kuwa amepanga kuhama nyumba hiyo.
Wawa ambaye kwa sasa anasumbuliwa na majeraha ya misuli aliyopata alipokuwa akitimiza majukumu yake wakati timu yake ikilazimisha sare mbele ya TP Mazembe uwanja wa Taifa kwenye mchezo wa hatua ya robo fainali Ligi ya mabingwa Afrika.
"Nawachukia wezi wamenifanya kitu kibaya, wamechukua kila kitu changu, kwenye kabati langu la mabegi wameacha mafuta tu, ila nguo zangu wamebeba, radio yangu kubwa na vitu vyangu vingi vya thamani, wamechukua, ila biblia wameniachia.
"Nimeripoti taarifa hizi polisi na ninawatafuta kweli yoyote niakayemuona ana kitu changu lazima nimpe adhabu kama ubayaubaya tu maana wameniumiza kweli," amesema Wawa.
Wawa alipatwa na mkasa huo wikiendi iliyopita ambapo amesema kuwa muda ambao wezi hao wanampukutishia vitu vyake alikuwa akipiga stori na kupata msosi na rafiki zake wa TP Mazembe wanaotoka Ivory Coast pamoja na mshikaji wake Tresor Mputu.
Dooooh wamemwachia boxer tyu🤣🤣🤣🤣🤣😂😂😂😂
ReplyDeleteNiltarajia wawa angekaa sehemu au nyumba yenye security camera. Ila mali ya wizi ni ya wizi tu na hatima ya mwizi ni kifo cha kinyama au jela.
ReplyDelete