April 12, 2019


JUMAPILI michuano ya Afcon kwa vijana chini ya miaka 17 itaanza kutimua vumbi rasmi huku Tanzania ikifungua panzia la michuano hiyo.

Tanzania itashuka uwanja wa Taifa majira ya saa 8:00 Mchana ambapo mpinzani wake atakuwa ni Nigeria.

Baada ya mchezo huo mchezo wa pili utakuwa ni kati ya Angola dhidi ya Uganda uwanja wa Taifa majira ya 11:00 jioni.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Mchezo Dk Harison Mwakyembe amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi kuipa sapoti timu ya Serengeti Boys.

"Mashabiki wajitokeze kwa wingi kuipa sapoti timu yetu ya vijana, pia mashindano yatakuwa na ushindani mkubwa kutokana na timu zote kujipanga," amesema Mwakyembe.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic