April 21, 2019


LEO ni Pasaka, vicheko na furaha vimetawala kwenye kambi ya wachezaji wa Ruvu Shooting, Mabatini baada ya kupewa posho ya Pasaka pamoja na mshahara wao mapema.
Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire ameliambia SportiXtra kuwa mambo ni mswano kwa wachezaji wote.
"Tumewatoa kambini kwanza wachezaji wetu wakale sikukuu na familia zao na watarejea Jumanne tuanze hesabu nyingine ila kwa sasa tumewaacha wafurahie matunda yao wakiwa na familia zao.
"Unajua Ruvu Shooting hapa sio pa mchezomchezo, wachezaji wanaskia tu na kusoma kuhusu njaa, maisha yao yametawaliwa na tabasamu, tumeshamalizana nao kwenye suala la mshahara achilia mbali posho ambazo tumewapa yaani wamejaa," alisema Bwire.
Ruvu Shooting ambao wapo nafasi ya 18 kwenye msimamo baada ya kucheza michezo 33 na kujikusanyia pointi 36 wataanza kuiwinda JKT Tanzania Jumanne baada ya kumaliza mapumziko waliyopewa na uongozi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic