NAHODHA wa Yanga, Ibrahim Ajibu amekuwa nje akitazama kikosi chake namna kinavyopambana kwenye michezo minne na anatarajiwa kuanza kazi rasmi kesho mbele ya Mtubwa Sugar.
Yanga ambayo ipo chini ya Kocha Mwinyi Zahera kwa sasa ni vinara wa ligi wana pointi 74 wakiwa wamecheza michezo 31 wameshinda michezo 23 wamepoteza michezo mitatu na wana sare tano.
Ajibu alikosa mchezo wa Yanga dhidi ya Lipuli FC uliopigwa uwanja wa Samora na Yanga ilipoteza kwa bao 1-0, pia mchezo wa Alliance Yanga ilishinda mabao 2-1, Ndanda FC Yanga ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1, African Lyon Yanga ilishinda kwa mabao 2-0 na Kagera Sugar ambao Yanga ilishinda mabao 3-2.
Kesho Yanga itashuka uwanja wa Jamhuri kumenyana na Mtibwa Sugar wakiwa na kumbukumbu ya kushinda mabao 2-1 mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa.








Andelee kukosa tu.bado Yanga inafanya vizuri sana
ReplyDelete