April 2, 2019


Kutokana na wachezaji nyota wa Simba Emmanuel Okwi na Clatous Chama kukosekana kwenye mchezo dhidi ya Mbao uliochezwa Uwanja wa Jamhuri kumekuwa na tetesi kwamba wachezaji hao wamejiengua ndani ya kikosi hicho jambo ambalo uongozi wa Simba umepinga.

Ofisa Habari wa Simba Haji Manara amesema kuwa wachezaji wake wote muhimu ambao wamekuwa wakihusihwa kuondoka ndani ya kikosi hicho ambao ni Chama na Okwi hawachomoki kwa sasa.

Manara amesema kwa sasa wachezaji wote wa Simba wapo kambini Morogoro wakijiandaa na mchezo wao wa kesho dhidi ya JKT Tanzania utakaochezwa Uwanja wa Jamhuri.

"Wengi wanasema wanaongea kuhusu wachezaji wetu wa Simba, niwaambie wazi kwamba Okwi na Chama wote wapo kambini Morogoro kwa sasa, hivyo hakuna klabu itakayowachukua kwa sasa ni mali ya Simba," amesema Manara.

Baada ya Simba kumaliza mchezo wao dhidi ya JKT Tanzania watarejea Dar kujiandaa na mchezo wa Ligi ya Mabingwa hatua ya robo fainali dhidi ya TP Mazembe.

2 COMMENTS:

  1. Hakuna Emanueli Okwii aliegoma au kujiengua Simba au Cletus Chama hawa wachezaji walikuwa kwenye majukumu yao ya timu za taifa lakini kinachoendelea ni usenge wa Kiandishi wa habari. Labda Simba kumekuwa na utulivu kwa kipindi sasa basi kuna watu hawaridhiswi na hali hiyo.

    ReplyDelete
  2. Ujinga jazz band.Wamekosa la kusema kuhusu Simba.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic