April 3, 2019


KOCHA Mkuu wa JKT Tanzania, Abdallah Mohamed 'Bares' amesema kuwa kazi yake ya kwanza leo atabeba pointi tatu muhimu mbele ya Simba ili kurejesha heshima ya JKT Tanzania.

Bares kabla ya kuinoa JKT Tanzania alikuwa kocha wa Prisons alipigwa chini kwa kile walichoeleza kuwa na matokeo mabovu, amejiunga na JKT Tanzania hivi karibuni akichukua nafasi ya Bakari Shime aliyesimamishwa kwa muda.

Bares amesema amekaa na timu kwa muda mfupi ila ana imani kwa mbinu alizowapa wachezaji wake pamoja na kuwasoma wapinzani wake mbinu zao ana uhakika ataibuka na pointi tatu muhimu.

"Muda mchache nimekaa na timu ila nimegundua wachezaji wana uwezo mkubwa na morali yao ipo juu, wapinzani wangu Simba nawatambua nimewafuatilia na kuzinasa mbinu zao hivyo hawanitishi ninaanza nao.

"Nimewaambia vijana, wachezaji wa kulindwa ni wote na sio kumtazama Bocco (John), Kagere (Meddie)  wala Chama (Clatous) bali ni timu nzima kwani wapinzani wetu wana mbinu nyingi ila hilo halinitishi," amesema Bares.

JKT Tanzania kwa sasa ipo nafasi 13 baada ya kucheza michezo 31 ikiwa na pointi 36, mchezo wao wa kwanza walipoteza nyumbani Mkwakwani kwa kufungwa mabao 2-0 dhidi ya Simba.

3 COMMENTS:

  1. Huyo mwengine lakini baada ya mchezo usikimbie

    ReplyDelete
  2. Hapa ndo utaona uwezo wa makocha wa kibongo na wa anga za juu, jaribu kufatilia mahojiano ya proffessional coach na hawa wetu wa kuungaunga utagundua kuna utofauti mkubwa sana wenzetu huwa wanaheshima sana timu inayokuzidi uwezo na kusema nitapambana lakin ni wazuri, mtazame patrick anavyozungumzia mchezo na mazembe anasema mazembe ni wazuri sana na ni wazoefu kwenye club bingwa, lakin hapo mbongo angekwambia mazembe ni timu ya kawaida sana halafu anapigwa anaanza visingizio vya marefa, maana amewaaminisha watu kuwa simba ni timu ya kawaida kwake.

    ReplyDelete
  3. Simba michezo 22 poont 57


    JK michezo 31 poiny. 36

    Napenda kumkumbusha anaejizatiti kuivurugia Simba

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic