MSHAMBULIAJI wa Simba, Meddie Kagere amefunguka kuwa atahakikisha anapambana kufa na kupona kwa kuwafunga wapinzani wao, TP Mazembe katika mchezo wa marudio kwa kuwa anataka kutimiza ndoto yake ya kutwaa kiatu cha ufungaji bora Afrika.
Kagere mwenye mabao sita akizidiwa bao moja na mshambuliaji wa Al-Nasr ya Libya, Moataz Al-Mehdi, ameyasema hayo kufuatia mchezo wa mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika Hatua ya Robo Fainali dhidi ya TP Mazembe ambao utapigwa kesho Jumamosi, Lubumbashi nchini DR Congo.
Kagere alisema amejipanga kupambana mwanzo mwisho kwa kuhakikisha Simba inafanikiwa kushinda mchezo huo huku yeye akitimiza ndoto yake ya kuwa mfungaji bora Afrika kutokana na mtu anayemzidi mabao timu yake kutolewa.
“Najua huu mchezo utakuwa mgumu lakini sisi tunakwenda kufuata ushindi kwa sababu ni jambo ambalo linawezekana kwetu, maana wachezaji wote tunaelewa umuhimu wa mchezo huo, sisi hatuangalii mechi zilizopita lakini watu wanatakiwa kuelewa kwamba hii ni robo fainali siyo hatua makundi, hivyo malengo ni tofauti ndiyo maana tunataka kushinda.
“Binafsi nitajitoa kupambana kutafuta mabao kwa ajili ya timu yangu lakini pia yataniwezesha kuwa mfungaji bora wa Afrika kwa sababu ambaye yupo juu yangu timu yake imeshatolewa, naamini nafasi ya kuwafunga TP Mazembe kwao ipo wazi,” alisema Kagere.
Kagere sawa lakini mechi hii ya Lubumbashi ni ya John Boko. Nasema mechi hii ni John Boko kwa sababu naamini kabisa anastahiki kupata hii nafasi ya kusahihisha alipoishia na kuwaziba midomo wanaomzodoa. Kwa matokeo yeyote yale Simba watakayoyapata kesho Lubumbashi basi watanzania na wanasimba tutayapokea kwa mikono miwili kwani timu ilishafanya makubwa kwenye mashindano haya na Asanteni sana Simba. Tukirudi kwa Boko,kama Mungu atamjalia kuamka vizuri basi cha kufanya kesho ni kuongoza mapambano sio tu kwenye fowadline ya Simba bali timu nzima kwani uwezo huo anao na wala hatakiwi kuuonea haya. Moja ya kazi kubwa ya Boko Lubumbashi kesho anatakiwa kujitahidi kuwa na umiliki mkubwa wa mpira miguuni mwake hasa katika eneo hatari na akiamua kufumua mishuti yake basi hapo ndipo anapotakiwa kuwa mmiliki mzuri wa akili yake ili kufanya maamuzi sahihi ili kupata matekeo chanya. Ni utulivu pekee na ari ya kupambana ya Kapteni Boko ndio itakaoweza kuikoa Simba Lubumbashi na si kagere si Okwi wala chama bali ni John Boko na hii ni kutokana na takwimu za mechi iliopita jijini Dar kati ya Mazembe na Simba ni kwamba John Boko alipambana hasa na kama angekuwa mtulivu wa kimaamuzi angalau katika nafasi mbili alizozipata basi leo watanzania tungekuwa tunazungumza lugha nyengine kabisa. Nnaimani kabisa bado Boko ana ari kubwa ya kupambana binafsi namtarajia kufanya makubwa sana Lubumbashi. Kila la kheri Simba.
ReplyDelete