April 20, 2019


MCHEZO wa leo wa Ligi Kuu kati ya Kagera Sugar na Simba ni moto wa kuotea mbali kutokana na rekodi za Kagera Sugar kuwaumbua wapinzani wao kwenye mchezo wao wa mwiho wa msimu wa mwaka 2017/18 kwa kuwafunga bao 1-0 mbele ya Rais, John Magufuli siku ya kukabidhiwa kombe la ligi.

Simba ina kumbukumbu ya kumshuhudia mshambuliaji wao ambaye alitwaa tuzo ya ufungaji bora msimu uiopita Emannuel Okwi akikosa penalti baada ya aliyekuwa langoni siku hiyo Juma Kaseja kupangua shuti dhaifu la Okwi.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara alijichanganya na video iliyosambaa ikionyesha namna alivyokuwa akiuliza swali namna hii " amepiga nani penalti Kaseja? aah Okwi,".

Simba hawajawa na rekodi ya kutisha mbele ya Kagera Sugar kwani wana kumbukumbu ya kupunguziwa kasi ya kutwaa ubingwa wao msimu wa 2016/17 baada kufungwa mabao 2-1 hali iliyowafanya Simba wapishane na ubingwa ukabebwa na wapinzani wao Yanga.

Kocha wa Kagera Sugar, Mecky Maxime amesema kuwa hana cha kuhofia leo mbele ya Simba atapambana kuizima kasi yao ya kubeba pointi tatu kwake kutokana na mbinu alizowapa wachezaji wake akiwa uwanja wa nyumbani Kaitaba.


"Nimejipanga na ninajua nacheza na aina gani ya timu sina mashaka katika hili muda utazungumza na kikubwa nachohtaji ni pointi tatu hakuna kingine," amesema Maxime.

Mbelgji wa Simba, Patrick Aussems amesema kuwa yupo tayari kupambana na vijana wa Kagera licha ya ushindani uliopo na kubanwa na ratiba atasepa na pointi tatu.

"Nimejiandaa kwa ajili ya kupata matokeo, vijana wangu wapo tayari kupambana na wanajua tunahitaji nini uwanjani, mashabiki waendelee kutupa sapoti kazi kubwa itamaliziwa na wachezaji uwanjani leo," amesema Aussems.

Kagera Sugar ipo nafasi ya 17 baada ya kucheza michezo 32 kibindoni imekusanya pointi 36 huku Simba ikiwa nafasi ya tatu baada ya kucheza michezo 23 kibindoni ina pointi 60.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic