April 20, 2019


LEO Uwanja wa Taifa, majira ya saa 10:00 jioni timu ya vijana chini ya miaka 17, Serengeti Boys itatupa kete yake ya mwisho kwenye mashindano hayo.


Tanzania ambao ni wenyeji wa michuano hii wanawakilishwa na Serengeti Boys ambao walianza kwa kuchechemea baada ya kufungwa mabao 5-4 mbele ya Nigeria na kupewa kichapo kingine cha mabao 3-0 mbele ya Uganda.

Kocha wa Serengeti Boys, Oscar Mirambo amebeba matumaini makubwa kwenye mchezo wa mwisho wa Kundi A dhidi ya Angola akiamini atashinda kufufua matumaini ya kusonga mbele.

"Mechi mbili za mwanzo tumeboronga baada ya kupoteza kitu ambacho hakikuwa kwenye matarajio ya watanzania wote na sisi pia tunajisikia vibaya kwa kuwavunja moyo.

"Bado tuna mchezo mmoja ambao ni muhimu sana kwetu kuweka heshima ya nchi yetu lakini pia inaweza kuwa daraja la kuishi matarajio ambayo tulikuwanayo mwanzo tuna imani kila kitu kinawezekana."

Leo Serengeti Boys wanacheza huku wakichungulia matokeo kati ya Nigeria na Uganda ambao nao wanacheza leo majira ya saa 10:00 jioni uwanja wa Chamazi ili kujaribu bahati yao kwa kutegemea maajabu ya soka huku dua ni Uganda ipoteze mbele ya Nigeria.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic