April 5, 2019


KIKOSI cha Kagera Sugar kilicho chini ya kocha mkuu, Mecky Maxime msimu huu kimepata taabu kwa Azam FC kwa kupigwa mara tatu bila wao kutikisa hata nyavu.

Kagera Sugar walianza kufungwa na Azam FC kwenye mchezo wa kwanza wa ligi uliochezwa Uwanja wa Kaitaba ambapo walikubali kufungwa bao 1-0.

Pia kwenye mchezo wa marudio Kagera Sugar walikubali kupoteza kwa kufungwa mabao 2-0 hali iliyowafanya wapoteze pointi zote sita mbele ya wapinzani wao hao.

Kabla ya mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa Nyamagana, Kagera Sugar walitolewa na Azam FC kwenye mchezo wa kombe la Shirikisho kwa kufungwa bao 1-0.

Hivyo kwa msimu huu Kagera Sugar imeshindwa kufurukuta mbele ya Azam FC kwa kuacha jumla ya pointi 6 huku wakifungwa jumla ya mabao manne.

Maxime amesema kuwa wameshindwa kupata ushindi katika michezo yao yote mbele ya Azam FC kutokana na safu ya ushambuliaji kushindwa kuwa makini.

"Wachezaji wanajituma uwanjani ila safu ya ushambuliaji ilishindwa kuzitumia nafasi ambazo wametengeneza, bado mapambano yanendelea hivyo tuna imani ya kufanya vizuri katika michezo yetu inayofuata," amesema Maxime.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic