HARUNA Shamte, beki wa Lipuli FC mfungaji pekee wa bao lililoipa pointi tatu mbele ya Yanga mchezo wa ligi kuu kwa kupiga faulo iliyozama kimiani na kumshinda Klaus Kindoki ameweka rekodi yake kwenye michuano ya kombe la Shirikisho.
Yanga itakutana na Lipuli kwenye hatua ya nusu fainali tena Uwanja wa Samora baada ya kuifunga Alliance hatua ya robo fainali penalti 4-3 hivyo wachetacheza na Lipuli ya Matola mkoani Iringa mwezi huu.
Shamte mpaka sasa ametupia mabao matatu kwenye kombe la Shirikisho huku mabao yote akiyafunga kwa kutumia mipira iliyokufa 'freekick' rekodi ambayo haijawekwa na mchezaji yoyote kwa sasa kwenye FA.
Alianza kufunga mabao mawili kwenye mchezo wake wa kwanza dhidi ya Laela ya mkoani Sumbawanga na akafikisha bao lake la tatu mbele ya Singida United tena kwa faulo, hivyo hizo ni salamu kwa Yanga watambue watakutana na washambuliaji wa aina gani.
Kocha Seleman Matola amesema huwa anampa mazoezi makali kijana huyo ili awe bora zaidi ya hapo hivyo anaamini atafanya mambo mengi makubwa ndani ya kikosi cha Lipuli.
"Anajua na kwene mazoezi huwa namfundisha namna ya kupiga mipira mingi iliyokufa, bado ana kasi na ni muelewa atafanya mengi kwa ajili ya timu," amesema Matola.
0 COMMENTS:
Post a Comment