KOCHA SIMBA ASEMA MECHI YA KESHO NI NGUMU LAKINI WANAHITAJI ALAMA TATU
Kocha Mkuu wa timu ya Simba, Patrick Aussems, amesema mechi ya kesho dhidi ya Alliance haitakuwa rahisi.
Aussems amesema mechi hiyo itakuwa ngumu kutokana uzuri wa Alliance namna ulivyo.
"Tunajua haitakuwa mechi rahisi sababu Alliance ni timu nzuri lakini sisi tumepoteza mchezo Bukoba na kesho tunataka alama tatu.
"Tunajua kwanini tulipoteza na tumejiandaa kwa hilo na ninaamini kesho tutakuwa vizuri."
0 COMMENTS:
Post a Comment