UBINGWA LIGI KUU UNAENDA SIMBA, TAMKO LATOLEWA
KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Aussems, amewataka mashabiki wa timu hiyo kutulia kufuatia matokeo mabaya katika mchezo wao dhidi ya Kagera Sugar kutokana na kuamini kuwa bado wana nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa msimu huu.
Aussems, raia wa Ubelgiji, ameyesema hayo kufuatia juzi Jumamosi, Simba kufungwa na Kagera Sugar mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera.
Aussems alisema kuwa kupoteza mchezo huo kumetokana na kuzidiwa na wapinzani wao lakini bado hakuwezi kumtoa katika mbio za kuwania ubingwa wa msimu huu katika Ligi Kuu Bara.
“Kiukweli matokeo hayakuwa mazuri kwa upande wetu, kwa sababu malengo ni kushinda kila mchezo ambao upo mbele yetu lakini wenzetu waliweza kutumia nafasi walizopata na ndiyo matokeo ya mpira.
“Kitu muhimu ni kwa mashabiki waendelee kutuunga mkono kwa sababu bado tuna mechi nyingi ambazo tunahitaji ushindi ili tuweze kufikia malengo ambayo tumejiwekea msimu huu, kwa kuwa naamini suala la ubingwa bado upo wazi kwetu kuweza kuchukua haijalishi tumepata matokeo ya aina gani,” alisema Aussems.
0 COMMENTS:
Post a Comment