April 12, 2019


KOCHA mkuu wa Simba, Patrick Aussems ameweka bayana kwamba John Bocco ataendelea kuwa chaguo la kwanza kwa wachezaji endapo itatokea suala la nani ambaye atapiga penalti za timu hiyo.

Kocha huyo mwenye miaka 54 ameyasema hayo ikiwa ni siku chache baada ya Bocco kukosa penalti kwenye mechi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika walipokuwa wakipambana na TP Mazembe.

Kocha huyo amesema kwake siyo jambo kubwa kwa nahodha wake huyo kukosa mkwaju huo kwani ni sehemu ya mchezo na huko nyuma alishafunga mipira hiyo mara nyingi.

“Siyo jambo kubwa kwa Bocco kukosa nafasi ile, kwenye soka ni wachezaji wengi sana walikosa nafasi kama hizo tena ikiwa ni muda ambao ulikuwa muhimu.

“Kwangu nafi kiri atabaki kama chaguo la kwanza kupiga penalti endapo tutapata nafasi hiyo, alishafunga mara nyingi huko nyuma hivyo sioni jambo lolote kwamba eti nimtoe kwa hilo hapa,” alisema kocha huyo raia wa Ubelgiji.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic