KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa anawaonea huruma wake wa wachezaji wake kutokana na kushindwa kukaa na familia kutokana na kubanwa na majukumu ya klabu hiyo.
Zahera amesema kuwa kubana kwa ratiba ya ligi kuu bara kunawafanya washindwe kupata muda wa kupumzika na familia.
"Nawaonea huruma wake wa wachezaji wangu kwa sababu hawapati muda wa kukaa na waume zao ambao muda wote wapo kambini wakijiiandaa na mechi.
"Ratiba sio rafiki kwetu kwa sabbau tulicheza na Alliance wiki iliyopita tukapanda ndege na kwenda Mtwara kucheza na Ndanda siku ya tatu yake tukarudi Mwanza kucheza na African Lyon pamoja na Kagera Sugar," amesema Zahera.
Kocha Mwinyi Zahera acha kulalamikalalamika andaa timu yako kukabiliana na changamoto hizo kwani yote hayo unayoyadai wahusika hawajawahi kuyatatua au kuyashughulikia kwa hiyo ni kazi bure kuyasema wewe endelea kukinoa na kukiandaa kikosi kwa ajili ya mechi na mashindano!
ReplyDelete