April 6, 2019



FT: Simba 0-0 Mazembe

Dakika 90 zimekamilika zinaongezwa dakika tatu kumaliza mchezo wa leo.

Dakika ya 80 Okwi anaonyeshwa kadi ya njano, milango bado ni migumu mpaka sasa.

Dakika ya 63 Jonas Mkude anaonyeshwa kadi ya njano.

Dakika ya 58 Nahodha wa Simba, John Bocco anapaisha penalti.
 Dakika ya 54 Chama alitolewa nje nafasi yake ikachukuliwa na Okwi.

Kwa sasa kipindi cha pili kimeanza Simba wanashambulia kwa kasi kwa Mazembe kutafuta bao la kuongoza ila milango bado ni migumu.

Mapumziko kwa sasa, hakuna mbabe.

Dakika 45 za kipindi cha kwanza zimekamilika na zinaongezwa dakika mbili.

Dakika ya 17 Mohamed Hussein wa Simba anaonyeshwa kadi ya njano baada ya kumchezea rafu mchezaji wa Mazembe.
  LIGI ya Mabingwa mchezo wa kwanza kwa Simba hatua ya robo fainali, unapigwa Uwanja wa Taifa dhidi ya TP Mazembe muda huu.

Kwa sasa ni kipindi cha kwanza huku mashabiki wa Simba wakiwa wamejitokeza wengi kuona namna itakavyokuwa Uwanja wa Taifa.

Mpaka sasa hakuna timu ambayo imeona lango la mpinzani wake ngoma ikiwa ni ngumu kwa timu zote.

Simba wanashambulia huku wapinzani wao Mazembe wakishambulia kwa kushtukiza.

4 COMMENTS:

  1. Safari inaishia Lubumbashiiiii,rekodi imevunjwa mtu kutoka salama kwa Mkapa

    ReplyDelete
  2. Lubambashi kutawaka moto kama Zamaleki ya Misri alipovuliwa Ubingwa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic