UONGOZI wa Simba umetoa tamko baada ya kubanwa mbavu na TP Mazembe kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa.
Simba leo wamelazimisha sare kwenye mchezo wao wa kwanza wa hatua ya robo fainali wakiwa nyumbani mbele ya TP Mazembe kwa kutoka suluhu bila kufungana.
Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara ametuma ujumbe kwa mashabiki wa Simba kupitia ukurasa wake wa Instagram na kuandika ujumbe uliosomeka namna hii:-
"Alhamdulillah,jitihada hazizidi kudra ila tuendelee kushikamana ktk Dakika tisini za Jasho na Damu kule Congo!!," amesema Manara.
Simba watarudiana na TP Mazembe ugenini ambapo ili apenye sasa anatakiwa akashinde ugenini akipigwa safari inaishia Congo, ngoma ikiwa droo mshindi anatafutwa kwa njia ya penalti.
Ngumu kumeza 😎
ReplyDeleteKituo kinachofuata ni Lubumbashi..........sijui kutakuwa na mafuriko au vipi!!
ReplyDeleteà ½Ã¸Ã ½Ã¸Ã ½Ã¸Ã ½Ã¸Ã ½Ã¸Ã ½Ã¸Ã ½Ã¸Ã ½Ã¸Ã ½Ã¸Ã ½Ã¸
ReplyDeleteMatamko fc
Dee la nguo,hakuna kitu na umesema wew hautaenda Congo mi nadhan team nzima tusienda🤣🤣🤣🤣🤣🤣
ReplyDeleteWaswahili husema kufanya kwa mara ya kwanza huwa sio kosa ila mkosaji anatakiwa kuchukua jitihada za makusudi kujirekebisha na asipofanya hivyo basi kitakachotokea ni muhusika kuja kushindwa kutimiza majukumu yake kabisa kwenye siku ambayo kila mtu anamtarajia.
ReplyDeleteSiku hii ilitarajiwa na wengi kuwasili kwani kutokana na kosakosa za magoli ya wazi kwa fowadi ya Simba kwenye mechi kadhaa muhimu kama si umahiri wa chama kuibeba fowadi yake ilikuwa haileti ishara nzuri kwa fowadi ya Simba. Simba walihitaji foward wa kazi alie makini hasa katika eneo la kumi nane. Sidhani kama Boko ni foward sahihi namba moja mbeba msalaba wa matarajio ya wachezaji wenzake ndani ya uwanja achilia mbali mashabiki. Sidhani kuwa ni aina ya foward wa kutekeleza wajibu wake ipasavyo kwenye mechi ambayo do or die. Boko ni mpamabanaji ila kwa sasa ni wa kusimamishwa kwenye maeneo ya assist tu na kutafutiwa mtupia nyavu makini.
ReplyDeleteIla mm nliona refa kama katubeba hv, ile ya okwi ilipaswa kuwa umeme ile nadhan, tumeanza kujua kucheza nyumban hakyanan maana huwa wanatutesa sana makwao
ReplyDelete