April 6, 2019


MASHABIKI wametakiwa kujitokeza kwa wingi Uwanja wa Karume kushuhudia soka safi la Ufukweni ambapo kwa sasa ligi inaendelea kila Jumamosi na Jumapili.

Akizungumza na Saleh Jembe, Mratibu wa Soka la Ufukweni, Kasana Jonathan amesema kuwa ni wakati wa mapinduzi kwa soka la ufukweni ambalo kwa sasa limeanza kujipatia umaarufu huku kila timu ambayo inashiriki ligi ikionyesha ushindani mkubwa.

"Kila timu inapambana na kuonyesha ushindani mkubwa, kila siku timu zinapambana na kufanya makubwa tofauti na jana hivyo mashabiki wajitokeze kwa wingi kuona vipaji vya kweli," amesema Jonathan.

Leo ligi iliendelea ambapo michezo mitatu ilipigwa kwenye uwanja maalumu uliopo Karume na matokeo yake ni kama ifuatavyo:-

Kisa FC imefungwa mabao 4-5 dhidi ya Savannah Boy.

Kijitonyama imeibuka na ushindi wa mabao 5-4 dhidi ya Friends Rangers.

Six Home City imeshinda mabao 6-2 dhidi ya Tabata Souls.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic