April 22, 2019


Mchekeshaji wa Ukraine, Volodymyr Zelensky amepata ushindi mkubwa katika uchaguzi wa urais baada ya kumshinda mpinzani wake, Petro Poroshenko, ambaye ndiye rais aliyekuwa madarakani.

Mchekeshaji huyo asiye na uzoefu wa kisiasa ameshinda kwa kishindo katika uchaguzi wa rais nchini Ukraine jana, na kupongezwa na viongozi mbalimbali  duniani.


Bwana Zelensky mwenye umri wa miaka 41, ameweza kumtoa madarakani rais Poroshenko ambaye amekubaliana na matokeo hayo.

Zelensky amekuwa akicheza mchezo wa kuigiza unaoitwa ‘Servant of the People ‘ ambapo amekuwa akiigiza kama kiongozi  anayetaka kuwa rais wa Ukraine.


Mchekeshaji huyo ameshinda kwa kunyakua asilimia 73 ya kura zote zilizopigwa, huku Poroshenko amepata asilimia 24 tu ya kura hizo lakini matokeo rasmi bado hayajatangazwa.

Kampeni za urais za Zelensky hazikuwa na mihadhara ya kijadi, badala yake mchekeshaji huyo alikuwa na hafla za vichekesho, pamoja na kuwavutia wapiga kura kupitia mitandao ya kijamii.

1 COMMENTS:

  1. Walimwengu wanasema seeing is believing yaani kukiona kitu kwa macho yako ni kuamini kwa kile unachokiona. Mtu ukiona kuu na kuridhika kuwa ni kuku halafu anakuja mtu na kukwambia hapana hakuwa kuku bali alikuwa Simba na wewe ukamkubalia kuwa kweli ni Simba basi ujue akili yako iko ISU na maafa yanaweza kukufika wakati wowote ule. Ukraine ilikuwa ni nchi nzuri tu na imara kiuchumi na kiusalama lakini shinikizo la nchi za magharibi kutaka mageuzi ya kisiasa nchini mwao kwa k
    ahadi ya demokrasia zaidi, maisha mazuri ziadi,uhuru zaidi, wakreinea wakaingia mtegoni kama wa Libya,kama wa Iraqi,kama wa Siria,kama Yemeni wakamshinikiza raisi aliekuwa madarakani kujiudhulu na kwa usalama wake akakimbilia Urusi la sivyo wangemuua. Waliimba na kucheza kwa furaha.kufarahia maisha mazuri ziadi ya ahadi kutoka kwa mabepari katika kipindi kifupi. lakini kila miaka ikienda mbele maisha ndani ya Ukraine yalizidi kuwa duni na duni.Nchi ikakatika vipande vipande,mauji ya wenyewe kwa wenyewe yakakisiri na wakabaguana wenyewe kwa wenyewe na kila kiongozi aliejitapa kuwa yeye ni mwanademokrasia mzuri zaidi wa kuleta maisha mazuri aliishia kujinufaisha yeye mwenyewe binafsi na kubakia kuwa kibaraka wa mataifa ya magharibi. Wayukreine wakaanza kujuta hadharani kwa waliyoyafanya na nadhani walikaa na kutafuta njia ya kueleza hasira zao kwa staili ya aina yake ili Dunia iwaelewe na iwe funzo kwa wengine na hasa kwa yale mataifa ya kibepari yaliyowaingiza mkenge. Na ndipo walipoamua kumchagua Kingwendu na kumbwaga raisi wao ambae ni mwanasiasa mzoefu na ni miongoni mwa mtu tajiri zaidi Ukraine ambae ni mshirika mkubwa pia wa mataifa ya magharibi. Nadhani kuleta shinikizo la kisiasa lenye lengo la kuleta mabadiliko ya uongozi wa nchi kwa kutumia nguvu na tashiwishi za mataifa ya nje ni jambo la hatari sana kwa usalama na ustawi wa Taifa husika kwani idadi ya mifano ya mataifa yaliyokwisha angamia kwa staili hii ni ya kutisha.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic