April 22, 2019


KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amemtaka Mkuu wa Idara ya Mawasiliano ya Simba, Haji Manara aache kumfuatilia kwa kuwa alichokisema yeye Zahera kuhusu Simba kuvuruga ratiba ya Ligi Kuu Bara ni kweli.

Zahera ameyasema hayo kutokana na Manara kuendelea kudai kuwa wao Simba hawataki kocha huyo kuendelea kuizungumzia Simba kila mara kwenye mahojiano yake.

Zahera alisema kuwa Manara hana nafasi ya kumzuia kuzungumza ukweli kwa kuwa timu yake (Simba) imekuwa ikihusika kuvuruga ratiba ya ligi kwa makusudi.

“Ninavyoizungumzia Simba na anachokisema yeye ni ukweli au uongo? Ukweli ni kuwa Simba inaweka rekodi ya dunia katika ligi, maana hata maofi sa wa Caf niliwaeleza juu ya ratiba yao (Simba), wakashangaa inakuwaje timu haichezi mechi za ligi hadi zinafikia kumi.

“Ingekuwa ni uongo yeye Manara angekuwa na sheria ya kunisema kama naisema vibaya timu yake, ila kama ninayoyasema ni ya ukweli basi Manara hana sheria ya kusema kuwa mimi ninawasema wao vibaya.

“Tatizo hajazoea kuambiwa ukweli, na hiyo ni shida kubwa kwake, hivyo asinitafute ubaya,” alisema Zahera

4 COMMENTS:

  1. Huyu kocha hajielewi kabisa utadhani afisa habar wa yanga

    ReplyDelete
  2. Acheni ushabiki, tunachotakiwa kufanya ni kujibu kauli za Zahera alizozisema kama ni kweli au la, vinginevyo tunaongea ushabiki zaidi ya ukweli. Inabidi tuongee kwa mifano, kwa mfano semeni kuwa TP Mazembe au Mamelod ambao wote wanashiriki Champion's league wanaviporo vingapi hadi sasa. Au tutolee mifano kwa timu nyingine Afrika au Ulaya ambazo zinaidadi sawa na Simba, na kama hakuna basi tujiulize kwa nini Simba? Au inawezekana udhaifu upo kwa Shirikisho letu la soka ambalo limeiwekea Simba viporo. Manara hana sababu ya kubishana na Zahera badala yake aongelee ukweli ama uongo wa Zahera. Tuache ushabiki na badala yake tuwe wawazi daima.

    ReplyDelete
  3. Simba anahusika vipi kuharibu ligi? Navyoelewa mie kuna kanuni zimewekwa na ni bodi ya ligi ndio wenye maamuzi ya mwisho kuyakubali maombi yanayoletwa na klabu kama vile kubadili viwanja na kueleza sababu za kufanya hivyo.lkn kocha Zahera yeye amekuwa mlalamikaji asiyeleweka na anacholalamikia.Yanga alivyopewa kipa umbele cha kucheza mechi 11 mfululizo ktk uwanja wake wa nyumbani hatukumsikia akilalamikia Simba au TFF kwa nini Yanga inacheza mechi 11 mfululizo uwanja wa nyumbani na haendi nje.Hii ilikuwa advantage kubwa kwa Yanga na wamenufaika kwa kushinda mechi zao karibu zote ktk mzunguko wa kwanza.Kuna baadhi ya timu zililalamika kwani nini Yanga acheze mechi 11 mfululizo DSM..sikumbuki kama kuna jibu lilotolewa toka Yanga au TFF au bodi ya ligi.Kwa mantiki hiyo Yanga alibebwa kiaina na Zahera analalamika tu kwa kujaribu kuficha madhaifu haya ya kubebwa na anatafuta sympathy kwa wanayanga.Simba atacheza viporo vyake kwa interval ya siku mbili lkn waliyataka wenyewe na wana advantage na disadvantage pia.Ni mahesabu yake ya kuhakikisha anashinda mechi 10 kati ya mechi 15 alizobakiza kuzicheza ili ampiku Yanga kama Yanga alivyokuwa na advantage ya kucheza mechi zake 11 mfululizo ktk uwanja wake wa nyumbani.Zahera alikuwa anajua hiyo advantage na ndio maana hakupiga kelele hivyo basi asitufanye kuwa wote ni mambumbu.Hesabu zake za kufikirika zimekataa.Anachopaswa Zahera ni kuombea Simba ipoteze mechi 5 ambazo bado shida kwa Simba kama Mtibwa, Azam, Prisons, Mbeya City, na Coastal Union au vinginevyo ajipange kwa ligi ya mwakani na hiyo FA cup.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic