April 22, 2019


KIKOSI cha Timu ya wanawake, Simba Queens leo kitashuka uwanjani kumenyana na Yanga Princess mchezo utakaochezwa saa 10:00 Jioni.

Timu hizi ambazo zote zinashiriki ligi ya Wanawake inayodhaminiwa na Serengeti Lite, zitashuka katika uwanja wa Karume, Dar es Salaam.

Simba inashuka uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kushinda mabao 7-0 mbele ya Yanga Princess mchezo uliopita ikiwa ni mzuguko wa kwanza.

Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Clifford Ndimbo amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi kuona namna ushindani ulivyomkubwa kwa sasa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic