April 4, 2019


Anayedai kuwa mmiliki wa Yanga, Juma Ali Mwambelo anaomba arejeshewe nafasi yake ya umiliki katika klabu hiyo ili aipatie Sh Bil.10 itakayotumika katika kuidhamini klabu hiyo.

Kauli hiyo, aliitoa jana kwenye Ofisi za Global Publishers inayochapisha magazeti ya michezo ya Championi na Spoti Xtra, Sinza-Mori jijini Dar es Salaam.

Yanga hivi sasa ipo kwenye mchakato wa uchaguzi. Akizungumza na Championi Jumatano, Mwambelo alisema anachotambua yeye bado ni mmiliki pekee wa klabu hiyo kwa mujibu wa katiba ya Yanga ya mwaka 1968.

Mwambelo alisema, anashangaa kuona uchaguzi ukiendelea kufanyika bila ya kufuata katiba ya mwaka 1968 inayotambulika mahakamani huku akiitaka Kamati ya Uchaguzi ya Yanga kufanya uchaguzi wake kwa kufuata katiba hiyo ya zamani na siyo ya mwaka 2011.

“Nipo tayari kwenda mahakamani kushtaki pamoja na kusimamisha uchaguzi wa Yanga, kutokana na kutumia katiba ya mwaka 2011 badala ya mwaka 1968, ambayo inatambulika kisheria na mahakama inafahamu hiyo. 

“Mimi ndiye mdhamini pekee ninayetambulika kikatiba, lakini wajanja walitumia ujanja kunizunguka na kunipokonya nafasi ya udhamini ya Yanga na kutotambua umiliki wangu, hivyo ninaomba nirejeshewe nafasi yangu ya udhamini.

“Niwahakikishie kuwa, nina uwezo wa kukusanya Sh Bil.10 kwa wiki moja kama nikirejea katika nafasi yangu ya udhamini Yanga na fedha hizo zitatokana idadi ya wanachama wapya 100,000 tutakaowasajili kwa kuchangia kiasi cha Shilingi 100,000 kwa muda wa siku tano tukitumia kadi za kisasa za ‘smartcard’,”alisema Mwambelo ambaye anadai kuwa na hati ya umiliki wa timu hiyo..

3 COMMENTS:

  1. Nyie waandishi acheni chokochoko mnatafuta baadhi ya wanachama wasio na maslahi na Yanga mnawafanyia mahojiano ili kuleta mtafaruku hizi mbinu chafu zinajulikana na wanaowatumia wanajulikana sasa hivi hamtaweza katiba ya 1968 kwanini itumike wakati uchaguzi zote zilizofanyika huko nyuma hazikutumia katiba hiyo anayoidai huyo Juma Mwambelo.....uchaguzi utafanyika kama ulivyopangwa na majority ya wanayanga, serikali, TFF, BMT, na Bodi ya Udhamini ya Yanga....hakuna na wala hawatakuwapo wa kuleta chokochoko....hakuna watu walioenda au watakaoenda mahakamani kwani watashughulikiwa na mkono wa serikali....nyie msilete mawazo ya kuchochea vurugu....hii ni amri ya mkuu wa nchi hakuna tena kuruhusu migogoro katika klabu kongwe!

    ReplyDelete
  2. hamna kitu hizo ni mbwembwe tu

    ReplyDelete
  3. Natafuta kitabu cha hadithi za abunuasi, Kama unayo naiomba

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic