April 19, 2019



UONGOZI wa timu ya Mtibwa Sugar umesema kuwa umelipa kisasi kwa wapinzani wao Yanga baada ya wao kuanza kuwafunga mzunguko wa kwanza Uwanja wa Taifa kwa mabao 2-1 nao wakashinda kwa bao 1-0 mchezo wa mzunguko wa pili uliochezwa Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema kuwa mwenendo mbovu wa timu ya Mtibwa kwenye mechi zao zilizopita uliwapa hasira wachezaji na kuamua kujituma kwa ajili ya timu yao.

"Unajua Mtibwa Sugar hatukuwa na mwenendo mzuri ghafla tu, nakumbuka tulishika mpaka nafasi ya 17 na 16 sasa kwa namna yoyote ile kwa timu bora lazima ishtuke na ifanye mabadiliko ya lazima kutafuta mafanikio.

"Haikuwa rahisi kupata ushindi mbele ya Yanga ila tulipambana na vijana walionyesha uwezo wao, sasa wao walitufunga mchezo uliopita kwao nasi tumewafunga kwetu na tumepanda mpaka kuwa nne bora kitu cha msingi sana kwetu," amesema Kifaru.

Mtibwa Sugar ipo nafasi ya nne kwenye msimamo baada ya kucheza michezo 32 imejikusanyia pointi 48.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic